http://3.bp.blogspot.com/-X5UFmDH0obY/UOaVkdBqPLI/AAAAAAAAScY/YHkKdRHVfnY/s640/WINO.bmp

G MOVIES CENTER DODOMA WAUZAJI WA MOVIES ZA KIJANJA ZA NDANI NA NJE YA NCHI TUPO BARABARA YA 6 NYUMA YA NMB BANK:HAJI MAPOWDER COSMETICS DODOMA NI BINGWA WA KUUZA VIPODOZI VYA IANA ZOTE NA PIA TUNATOA USHAURI JUU YA NGOZI YAKO, DUKA LIPO BARABARA YA 6 NA JINGINE BARABARA 8: TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0716909567 NA 0766909567 AU TUMA BARUA PEPE bossngasa@gmail.com.:THE BEST BLOG IN DODOMA:

Monday, 3 September 2012

Mabaki ya Mwili wa Mwandishi wa Habari Daudi Mwangos Alie uwawa jana

Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake.





Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini.


Daud Mwangosi ameuwawa jana katika vurugu za Polisi na wafuasi wa CHADEMA katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa.
Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za CHADEMA Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.
Kabla ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadaye mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa CHADEMA kurushiana mawe kwa mabomu, zaidi ya magari matano ya CHADEMA na ya wananchi yameharibiwa, huku watu kadhaa wakiachwa wamejeruhiwa hali mwanahabari mmoja, Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Source: http://francisgodwin.blogspot.com/

Marehemu Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.       

No comments: